|
|
|||
|
||||
Overview"DIWANI hii ya N'na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini ilishinda kwenye awamu ya kwanza ya Tuzo za Fasihi ya Afrika kwa Lugha ya Kiswahili inayotolewa na Wakfu wa Mabati-Cornell mwaka 2015. Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015. Hii ni miaka mitano ya mwanzo ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani - mbali na nyumbani kwao, Zanzibar. Ndani yake, kwa hivyo, muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kujitambulisha nayo zaidi na zaidi. Ndipo hisia za kutambuwa kuwa ana kwao zinapopanda kiwango cha juu. Kutoka kipembe cha mbali, Mohammed Ghassanani anakuangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani: ""Samaki hajijui kuwa amerowa!"" Na sababu ya kutokujijuwa huko, kwa hakika, ni kwa kuwa yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote." Full Product DetailsAuthor: Mohammed GhassaniPublisher: Lulu Press Inc Imprint: Lulu.com Dimensions: Width: 15.20cm , Height: 0.80cm , Length: 22.90cm Weight: 0.195kg ISBN: 9781470942892ISBN 10: 1470942895 Pages: 126 Publication Date: 27 September 2021 Audience: General/trade , General Format: Paperback Publisher's Status: Active Availability: In stock We have confirmation that this item is in stock with the supplier. It will be ordered in for you and dispatched immediately. Language: Swahili Table of ContentsReviewsAuthor InformationMohammed Ghassani alizaliwa kisiwani Pemba mwaka 1977, ambako alikulia na kusomea hadi alipohamia kisiwani Unguja kwa ajili ya masomo na maisha mwaka 1996 na mwaka 2010 akahamia nchini Ujerumani, ambako ndiko anakoishi na kufanya kazi. Tab Content 6Author Website:Countries AvailableAll regions |