|
|
|||
|
||||
OverviewMAISHA YANGU: KHAINI AU MUHANGA WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR? ni kitabu kinachoeleza historia ya Zanzibar ya hivi karibuni na vipi Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika ulivyoanzishwa hadi kuwepo taifa jipya la TANZANIA. Khamis Abdulla Ameir amejaribu kwa kadri ya uwezo wake kuweka sawa historia ya Muungano wa Tanzania katika njia iliokuwa sahihi kabisa, ili Watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo, waweze kuelewa chanzo na malengo halisi ya Muungano huu. Kitabu hiki kinasimulia historia mpya ya kileo kuhusu vipi vyama vya siasa vilivyoanzishwa Zanzibar tokea mwanzoni mwa miaka ya 1950 na vipi vyama hivyo na vyama vya wafanyakazi vilivyodai uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Balozi Mkaazi wa Uingereza na sio kutoka kwa Mfalme Mwarabu ambaye alikuwa hana sauti mbele ya Balozi wa Uingereza. Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Disemba, 1963 na serikali ya mseto ya ZNP/ZPPP ikakabidhiwa madaraka baada ya kushinda katika uchaguzi. Mwandishi anaeleza vipi Mapinduzi ya Zanzibar yalivyotekwa nyara na Mabeberu wa Uingereza na Marekani kwa kushirikiana na Viongozi wakuu wa Kenya, Uganda na Tanganyika ili Zanzibar isiweze kutekeleza siasa ya Kisoshalisti, ambayo nchi hiyo ilishaanza kuitekeleza kivitendo. Frank Carlucci, jasusi maarufu wa CIA, alipelekwa Zazibar na serikali yake kwa kazi moja tu, nayo ni kuizuia Zanzibar isijekuwa CUBA YA AFRIKA na kuziambukiza siasa ya Usoshalisti nchi jirani za Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Kitabu kilichapishwa na DL2A Buluu Publishing, jijini Paris, Ufaransa. Full Product DetailsAuthor: Khamis Abdulla AmeirPublisher: Diffusion Des Litteratures En Langues Africaines Imprint: Diffusion Des Litteratures En Langues Africaines Dimensions: Width: 14.80cm , Height: 4.10cm , Length: 21.00cm Weight: 0.934kg ISBN: 9791092789232Pages: 588 Publication Date: 25 March 2022 Audience: General/trade , General Format: Paperback Publisher's Status: Active Availability: In stock We have confirmation that this item is in stock with the supplier. It will be ordered in for you and dispatched immediately. Language: Swahili Table of ContentsReviewsAuthor InformationHadithi ya maisha ya Khamis Abdulla Ameir siyo ya kubuni bali ni ya kweli kabisa juu ya mambo yaliyotokea Zanzibar katika kipindi cha kilele cha Vita Baridi, COLD WAR, baina ya nchi za kibepari za Magharibi na zile za kikomunisti za Mashariki. Khamis aliweza kufika London, Uingereza. Huko ndiko alipojitambulisha na kuwa muumini wa siasa za mrengo wa kushoto baada ya kukutana na akina Abdulrahman Mohammed Babu na Ali Sultan Issa na kuhudhuria mikutano na makongamano yaliyokuwa yakiandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha Uingereza na huku akijishughulisha kuwasaidia baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Afrika Mashariki waliokimbilia London kuendelea na harakati zao za kuzikombowa nchi zao ili zipate uhuru. Aliporejea Zanzibar, kabla na baada ya Mapinduzi, Khamis alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi (FPTU). Khamis alikuwa Mjumbe katika Baraza La Mapinduzi (BLM) kwa muda wa miaka minane mfululizo. Alikuwa vile vile Mwenyekiti wa taasisi kadhaa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kwa hivyo, aliyajuwa mambo mengi yaliyokuwa yakifanywa na SMZ, mazuri na mabaya. Yote ameyaeleza kwa ufasaha mkubwa katika kitabu hiki. Pia, Khamis anaeleza jinsi Hati ya Makubaliano ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilivyoshindwa kupata ridhaa ya BLM na kusababisha Zanzibar kupoteza uhuru wake kamili wa kujiamulia mambo yake yenyewe. Khamis alikamatwa na kutiwa jela chini ya ukatili wa Mandera (Ba Mkwe), mtesaji maarufu wa watu mahabusi. Aliishi jela kwa muda wa karibu miaka 7 baada ya kuuawa Rais Abeid Amani Karume na yeye kusukumiziwa janga la uhaini. Tab Content 6Author Website:Countries AvailableAll regions |